Yanga bado inapambana kumbakisha Aziz Ki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jun 2024
Yanga bado inapambana kumbakisha Aziz Ki

Yanga bado iko kwenye majadiliano na kiungo mshamuliaji Stephane Aziz Ki kwa ajili ya kumuongezea mkataba

Wananchi wana matumaini ya kushinda vita ya kumbakisha Aziz Ki kwa kuwa Mburkinabe huyo anafurahia maisha yake Jangwani. Mpaka mwishoni mwa wiki hii, hatma ya Aziz Ki itakuwa imefahamika

Baada ya Mamelodi Sundowns na Kaizer Chiefs sasa klabu ya Pyramids Fc nayo imengia vitani kumtaka Aziz Ki

Msimu uliopita Pyramids walifanikiwa kumsajili Fiston Mayele na inaonekana wamedhamiria pia kumng'oa Aziz Ki Jangwani

Hata hivyo haitakuwa mara ya kwanza kwa Pyramids Fc kujaribu kumsajili Aziz Ki. Wakati Aziz Ki anasajiliwa na Yanga misimu miwili iliyopita, Pyramids ni miongoni mwa timu zilizotuma ofa nono zaidi ya Yanga lakini Aziz akachagua kujiunga na Yanga baada ya ushawishi wa Rais Injinia Hersi Said

Injinia Hersi aliahidi kuwa uongozi wake utafanya kila linalowezekana kuhakikisha wachezaji wote muhimu akiwemo Aziz Ki wanabaki

Tayari Yanga imeshinda vita ya kumuongezea mkataba Kocha Miguel Gamondi ambaye jana aliwathibitishia Wananchi ameongeza mkataba wa mwaka mmoja

Gamondi ataendelea na benchi lake la ufundi ambalo msimu uliomalizika limeiwezesha Yanga kutetea ubingwa wa ligi kuu, kombe la FA na kucheza robo fainali ya ligi ya mabingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’