Kiungo mshambuliaji wa Yanga Augustine Okrah anaweza kupewa mkono wa kwaheri ikiwa ni miezi sita tangu ajiunge na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya NBC 2023/24
Okrah alitua Yanga mwezi Januari akitokea klabu ya Bechem United ya Ghana ikiwa ni mara ya pili kwake kucheza ligi ya Tanzania Bara baada ya kuitumikia Simba
Hata hivyo mwanzo wake na Yanga haukuwa mzuri baada ya kupata majeraha ya kuchanika 'mgomba wa pua' katika michuano ya kombe la Mapinduzi ambayo yalimuweka nje kwa takribani wiki sita kabla ya kuanza kucheza huku akivaa mask
Hata baada ya kupona majeraha hayo ikawa sio rahisi kwake kupenya katika kikosi cha kwanza kutokana na ushindani uliopo
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi alimtumia katika baadhi ya mechi lakini ni kama hakumshawishi Muargentina huyo kwani alimuondoa kabisa katika mipango yake kwenye mechi za mwishoni mwa msimu
Hatma yake imebaki mikononi mwa mabosi wa Yanga lakini haitashangaza kama atakosekana katika kikosi cha Yanga msimu ujao