Ulikuwa msimu wa maokoto kwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Jun 2024
Ulikuwa msimu wa maokoto kwa Yanga

Bado mashabiki wa Yanga hawajapoa na shamrashamra za ubingwa wa kombe la Shirikisho la CRDB ambao Yanga walitwaa juzi baada ya kuifunga Azam Fc mikwaju ya penati 6-5 kufuatia matokeo ya suluhu ya bila kufungana

Hilo lilikuwa taji la pili kwa Yanga kutwaa msimu huu baada ya lile la Ligi Kuu walilotwaa wiki chache zilizopita wakishinda mataji yote mawili kwa misimu mitatu mfululizo

Mafanikio haya yameingiza fedha za maana katika akaunti ya Yanga fedha ambazo pasipo na shaka zinawapa jeuri mabosi wa Yanga na pengine cheche zake zitaonekana katika dirisha la usajili

Ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu umeihakikishia Yanga kuvuna jumla ya Tsh Milioni 600 ambapo Milioni 100 zimetoka kwa wadhamini NBC na Milioni 500 zikitoka kwa Azam Media

Lakini pia ubingwa huo umeipa tena Yanga kiasi cha Sh 150 milioni kutoka kwa wadhamini wao wakuu, kampuni ya SportPesa kwenye mkataba wao, makubaliano ya Yanga na kampuni hiyo ni kwamba kama itatwaa ubingwa itapewa bonasi ya kiasi hicho cha fedha.

Hatua ya kulichukua taji la CRDB inaifanya Yanga ivune tena kiasi cha Sh 112 milioni kutoka kwa wadhamini wao hao wakuu wa SportPesa

Ubingwa huo wa shirikisho pia unaifanya Yanga imevuna Tsh Milioni 200 kutoka kwa Wadhamini wakuu wa michuano hiyo, CRDB Bank

Yanga pia iliingia mkataba binafsi wa maudhui na matangazo ya televisheni na Azam Media ambao kwa hatua ya kuchukua ubingwa tu imejihakikishia kiasi cha Sh 1.1B

Pia kuna makusanyo kutoka Ligi ya Mabingwa ambapo Yanga imevuna takribani Bilioni 2.3 baada ya kufika robo fainali

Yanga imevuna zaidi ya Sh4.5 Bilioni kutoka kwa wadhamini mbalimbali na hii ni nje ya fedha za mapato ya mauzo ya jezi, GSM na usajili wa mashabiki na wanachama

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’