Yanga kuifuata Welayta Dicha Jumapili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Apr 2018
Yanga kuifuata Welayta Dicha Jumapili
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka keshokutwa Jumapili kuelekea nchini Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Wolaitta Dicha kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Mchezo huo utapigwa katika mji wa Hawassa Jumatano ijayo April 18. Mji huo uko umbali wa kilometa 275 kutoka mji Mkuu wa nchi hiyo Addis Ababa.

Yanga inakwenda Ethiopia ikiwa tayari na mtaji wa mabao 2-0 iliyopata kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa April 07 kwenye uwanja wa Taifa.

Inahitaji ushindi, sare au kufungwa kwa tofauti isiyozidi mabao mawili ili iweze kufuzu.

Kama itapata goli la ugenini itakuwa imejiweka kwenye nafansi nzuri zaidi ya kutinga hatua ya makundi kwani itailazimu Dicha kushinda zaidi ya mabao matatu.

Katika mchezo huo Yanga itakuwa na wachezaji wake wanne, Kelvin Yondani, Said Juma Makapu, Obrey Chirwa na Papi Tshishimbi waliokosa mchezo uliopita wakitumikia adhabu ya kadi mbili za njano.

Makocha Noel Mwandila na Shedrack Nsajigwa nao watarejea katika benchi baada ya kukaa jukwaani mchezo uliopita kutokana na mkanganyiko uliosababishwa na CAF.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’