Mkude, Guede kamili kuikabili Azam Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 May 2024
Mkude, Guede kamili kuikabili Azam Fc

Daktari wa Yanga Dk Moses Etutu amesema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Azam Fc utakaopigwa Jumapili

Etutu amesema wachezaji Jonas Mkude na Joseph Guede waliokuwa changamoto za maradhi wote wako tayari na wameungana na wachezaji wenzao

Etutu amesema wachezaji hao wanashiriki mazoezi na wachezaji wenzao baada ya kikosi kufika Zanzibar.

"Kwa ujumla wachezaji wote hali zao kiafya ni wazima, tumekuwa na wachezaji wawili (Mkude, Guede) ambao walikuwa na shida kidogo kama kuumwa malaria na homa lakini wameanza mazoezi vizuri"

"Hali ya hewa hapa ni upepo na kibaridi kidogo kulinganisha na Dar es Salaam, lakini sidhani kama hali hii itabadilisha mabadiliko ya kimwili kwa wachezaji, pengine inaweza kutusaidia kupunguza uchovu na kuwafanya wachezaji wasichoke mapema, hivyo ni hali ya hewa nzuri na haina madhara kwa wachezaji," alisema Etutu

Yanga ilitua Zanzibar jana na moja kwa moja kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Azam Fc utakaopigwa Jumapili katika uwanja wa New Amaan Complex

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’