Jana Stephane Aziz Ki alikamilisha msimu wa Wananchi kwa furaha baada ya kuiongoza Yanga kupata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Tanzania Prisons
Katika mchezo huo, Aziz Ki alifunga mabao matatu 'hat-trik' na kufanikiwa kuondoka na tuzo ya mfungaji bora akifikisha mabao 21 akimuacha Feisal Salim na mabao 19 akiwa nafasi ya pili
Tuzo hii ya Aziz Ki imekuja na rekodi za aina yake. Aziz Ki ametumia mechi chache kufunga mabao 21 kulinganisha na watangulizi wake katika misimu ya karibuni
Katika msimu uliofika tamati jana, Aziz Ki alikamilisha mechi 27 na kufunga mabao 21 pamoja na kutoa assist nane
Katika misimu 20 iliyopita, ni Meddie Kagere pekee aliyefunga mabao mengi kumzidi Aziz Ki, akifunga mabao 23 na 22 lakini katika msimu uliokuwa na mechi 38
Amissi Tambwe nae aliwahi kumaliza msimu na mabao 21 ambayo aliyafunga katika msimu wenye mechi 38
Bado rekodi ya mabao inashikiliwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga Mohammed Hussein 'Mmachinga' aliyefunga mabao 26 katika mechi 24 tu