Tuwaondoe kwanza Dicha, mengine baadae

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Apr 2018
Tuwaondoe kwanza Dicha, mengine baadae
Kumekuwa na 'vuguvugu' ndani ya klabu ya Yanga baada ya kujiondoa kwa Kocha Mkuu George Lwandamina kutokana na sababu zake alizoeleza.

Juzi baada ya mchezo dhidi ya Singida United Kamati ya Utendaji ya Yanga ilikaa kikao cha dharura kujadili sintofahamu iliyojitokeza baada ya kujiondoa kwa Lwandamina.

Leo viongozi wa Yanga walitarajiwa kufanya Mkutano na Waandishi wa habari, hata hivyo Mkutano huo umeahirishwa kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.

Kimsingi nafikiri kuahirishwa kwa Mkutano huo kumefanywa kwa nia njema.

Ikumbukwe Yanga ina mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho Jumatano ijayo dhidi ya Welayta Dicha nchini Ethiopia.

Nadhani ni vyema kwa WanaYanga kuwa wamoja kuhakikisha timu inapata matokeo kwenye mchezo huo wa marudiano ili iweze kutinga hatua ya makundi.

Ukiachana na swala la kutetea ubingwa wa VPL, mafanikio katika michuano hii ya CAF yafaa iwe kipaumbele zaidi.

Yanga imebakisha dakika 90 tu kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Kama itatinga hatua hiyo, pesa watakazolipwa na CAF ni nyingi na zitaisaidia kutatua baadhi ya changamoto zake.

Wakati huu yafaa WanaYanga wawe wamoja kuisaidia timu yao isonge mbele.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’