Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amewataka mashabiki na Wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa leo katika Jumamosi ya Mabingwa
Aziz Ki amesema leo ni siku maalum kwa Yanga hasa mashabiki ambao wamekuwa na timu tangu siku ya kwanza ya msimu
Kinara huyo wa mabao ligi kuu msimu huu amesema mafanikio yoyote waliyopata kama timu yametokana na sapoti ya mashabiki
Aidha Ki amebainisha kuwa leo ni siku nyingine ya kuvunja rekodi akiahidi kufunga katika mchezo dhidi ya Tabora United
"Leo ni maalum kwenu Wananchi! Unaipenda timu hii, umeiombea, na umeifuata kwenye kila uwanja ili kuonyesha msaada wako kama mtu wa 12 wa mwisho"
"Sote tunakungoja kwenye uwanja kusherehekea pamoja kwa sababu, hii ni kwa ajili yako. Bila usaidizi wako, tukisengeza kupata mafanikio haya. Njoo ujiunge nasi ili tuweze kukushukuru kwa njia yetu maalum uwanjani, na kisha kucheza pamoja katika sherehe," aliandika Aziz Ki katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Aziz Ki anawania tuzo ya ufungaji bora akiongoza mbio na mabao yake 17, akifuatiwa kwa karibu na Feisal Salum mwenye mabao 16