Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki jana alifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 4-0 ambao Yanga waliupata dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Mabao hayo yalimfanya Aziz Ki arejee katika usukani wa kuwania ufungaji bora msimu huu baada ya kufikisha mabao 17
Aziz Ki sasa amefikia rekodi ya mabao 17 ambayo mshambuliaji wa zamani wa Yanga Fiston Mayele alifunga msimu uliopita na kuibuka mfungaji bora akigawana tuzo hiyo na Saido Ntibazonkiza wa Simba
Ki ana dakika 180 za kuvunja rekodi hiyo na pengine kuandikisha rekodi yake mpya ya mabao
Naye kiungo kiraka Maxi Nzengeli jana alifunga bao lake la 10 msimu huu na kusogea katika nafasi ya nne kwenye orodha ya wafungaji
Mudathir Yahya anafuatia akiwa amefunga mabao 9, Pacome Zouzoua amefunga mabao 7 huku Clement Mzize akifikisha mabao 6 jana
Joseph Guede amepachika mabao matano wakati Kennedy Musonda akiwa na mabao manne
Nyota wengine wa Yanga waliofunga bao moja msimu huu ni Dickson Job, Skudu, Augustine Okrah, Yao Kouassi na Hafiz Konkoni ambaye ametimkia Libya