Michezo ya ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 24 imeendelea leo katika viwanja mbalimbali.
Mchezo kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Azam FC uliokuwa upigwe leo kwenye uwanja wa Mabatini umeahirishwa baada ya uwanja kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.
Mchezo huo sasa utapigwa kesho Ijumaa, April 13.
Matokeop ya michezo mingine iliyopigwa leo, Simba imeilaza Mbeya City mabao 3-1 wakati Mtibwa Sugar imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC.
Ushindi wa Simba unaifanya ifikishe alama 55 hivyo kuongoza ligi kwa tofauti ya alama nane.
Hata hivyo Simba imecheza mchezo mmoja zaidi ya Yanga. Jumatatu ijayo inatarajiwa kuongeza mchezo mwingine itakapoikabili Tanzania Prisons uwanja wa Taifa.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na TFF, Yanga haitakuwa na mchezo wa ligi mpaka April 29 itakaposhuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Simba kwenye mchezo wa watani wa jadi.
Yanga inatarajiwa kuondoka wikiendi hii kwenda nchini Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho dhidi ya Wolaitta Dicha

ADVERTISE HERE