Julai 21 2022, aliyekuwa Msemaji wa Yanga Haji Manara alikumbana na rungu la TFF akifungiwa miaka miwili na faini ya Tsh Milioni 20
Ni baada ya lile sakata la kurushiana maneno baina yake na Rais wa TFF Wallace Karia katika mchezo wa fainali kombe la FA mkoani Tanga, Yanga ikifanikiwa kubeba taji hilo kwa ushindi wa mikwaju ya penati 4-1 kufuatia matokeo ya sare ya mabao 3-3
Manara alikata rufaa ambapo matokeo ya rufaa hiyo alipunguziwa faini kutoka Tsh Milioni 20 na kutakiwa kulipa Tsh Milioni 10 huku kifungo cha miaka miwili kikibaki palepale
Hatimaye itakapofika mwezi Julai mwaka huu, Manara atamaliza kifungo chake na kurejea katika majukumu yake kama zamani
Manara ameahidi kuwa atarejea kuisemea Yanga akiwa na ari kubwa kwani miaka miwili aliyokuwa nje imemuongezea maarifa
"Nitarejea nikiwa na ari kubwa na nitaendelea pale pale nilipoishia na kwa kasi zaidi,kukaa nje kipindi kirefu kumenipa maarifa makubwa ya kujua nini nifanye kuisaidia klabu yangu," alisema Manara
Bila shaka Wiki ya Mwananchi ya mwaka huu itafana zaidi kwani Manara atarejea kuwaongezea nguvu kina Ali Kamwe katika kufanikisha tukio hilo kubwa la kukaribisha msimu mpya