Mkwasa asihusishwe kuondoka kwa Lwandamina Yanga

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
12 Apr 2018
Mkwasa asihusishwe kuondoka kwa Lwandamina Yanga
Kuondoka kwa kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina kunatumiwa na baadhi ya vyombo vya habari 'kuvuruga' amani iliyopo katika uongozi wa Yanga.

Baadhi ya mitandao imemuhusisha Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa kuwa chanzo cha Lowandamina kuondoka, jambo ambalo sidhani kama lina ukweli wowote.

Wanaosema kuwa sababu ni Mkwasa alitaka apewe jukumu la kuinoa Yanga sidhani kama wako sahihi kwa kuwa Mkwasa alikuwepo Yanga akiwa Katibu Mkuu kabla ya Lwandamina.

Kama alitaka nafasi ya ukocha angeweza kuipata wakati ule alipoachana na majukumu ya kuinoa timu ya Taifa lakini akaamua kukubali majukumu ya Ukatibu Mkuu.

Mkwasa ndio 'engine' ya Yanga kwa sasa. Akishirikiana na vingozi wengine, ndio wanaosukumu kufanya mabadiliko ili kuifanya Yanga iwe na nguvu ya kiuchumi.

Sio siri Yanga imekumbwa na changamoto nyingi, kama sio akina Mkwasa pengine Lwandamina angekuwa ameondoka muda mrefu sana.

Jambo jingine la msingi hapa ni lazima ifahamike kuwa mkataba wa kocha George Lwandamina kuifundisha Yanga unamalizika mwishoni mwa msimu kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi.

Hivyo kama Lwandamina ameamua kuondoka basi ni kwa utashi wake mwenyewe, hakutaka kuongeza mkataba mwingine.

Na hata taarifa iliyotolewa na ZESCO wakati wakimtangaza Lwandamina wamesema kocha huyo ataanza majukumu yake mwishoni mwa mwezi wa tano.

Hivyo nao wanafahamu bado ana mkataba na Yanga lakini kwa kuwa unaelekea ukingoni habanwi kusaini mkataba wa awali huko ZESCO.

Ninachofahamu kama ZESCO watahitaji huduma ya Lwandamina mapema zaidi ni lazima waje wamalizane na Yanga.

Kwa vyovyote lazima kuwe na makubaliano kati ya uongozi wa Yanga na ZESCO/Lwandamina ili kumruhusu aweze kuanza kuitumikia ZESCO sasa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’