Yanga Bingwa Ligi Kuu 2023/24

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 May 2024
Yanga Bingwa Ligi Kuu 2023/24

Yanga imetetea taji lake la ligi kuu kwa msimu wa tatu mfululizo baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliopigwa uwanja wa Manungu

Mtibwa Sugar walitangulia kupata bao kupitia Charles Ilanfya mapema katika kipindi cha kwanza hata hivyo ubora wa Yanga ukaamua mechi kwenye kipindi cha pili kwa mabao ya Kennedy Musonda, Clement Mzize na bao jingine likiwa la kujifunga mlinzi wa Mtibwa Sugar

Akizungumza baada ya ubingwa huo wa 30, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amewapongeza wachezaji na uongozi bila kuwasahau mashabiki ambao wamekuwa bega kwa bega na timu tangu mwanzo wa msimu

Gamondi amesema wamedhihirisha kwa vitendo kuwa timu bora Tanzania wakizifunga timu zote 15 zinazoshiriki NBC Premier League msimu huu

"Nawapongeza wachezaji, viongozi pamoja na Wananchi wote kwa ubingwa huu. Haikuwa rahisi lakini kwa umoja wetu na ushirikiano, tumefanikiwa"

"Tumekuwa mabingwa tukiwa mechi tatu mkononi lakini pia tumezifunga timu zote 15 zinazoshiriki ligi tukiwa timu iliyoshinda mechi zote nyumbani mpaka sasa"

"Ni ni rekodi na heshima kubwa kwangu huu ukiwa msimu wa kwanza. Haya ni mafanikio ya Yanga kama timu na sio mimi tu," alisema Gamondi

Wananchi wameanza shamrashamra katika uwanja wa Manungu. Sherehe kubwa itakayoambatana na Parade la Ubingwa itafuatia...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’