Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi leo anaiongoza timu yake katika mchezo muhimu wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa katika uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro
Huu ni mchezo muhimu kwa Gamondi na Yanga kwa ujumla kwani matokeo ya ushindi yataihakikishia Yanga kutwaa ubingwa. Litakuwa taji la kwanza kwa Gamondi katika msimu wake wa kwanza na Yanga
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said atakuwa mtu mwenye furaha zaidi katika ubingwa huo kwa sababu ni yeye aliyefanikisha ujio wa Gamondi ambaye wakati anatua hakuna mtu aliyekuwa akimfahamu
Baada ya Kocha Nasreddine Nabi kuondoka, wengi waliamini ulikuwa mwanzo wa Yanga kuyumba, lakini mpaka sasa Gamondi amefanya zaidi ya kile alichofanya Nabi katika msimu wake wa kwanza
Leo Gamondi anaweza kuiongoza Yanga kutwaa ubingwa mapema zaidi kuliko msimu uliopita kwani kama Yanga itashinda leo itakuwa bingwa huku ikiwa na mechi tatu mkononi
Bila shaka uongozi wa Yanga tayari umemuandalia Gamondi mkataba wa muda mrefu kwani alipotua alisaini mkataba wa mwaka mmoja uliokuwa na kipengele cha kuongeza mwingine kwa kuzingatia masharti
Moja ya mashrti ni kutwaa ubingwa wa ligi ambao sasa ni suala la muda tu, ataurejesha Jangwani
Gamondi pia alifanya vyema katika michuano ya ligi ya mabingwa akiipeleka Yanga hatua ya makundi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25
Lakini hakuishia makundi tu, Gamondi akahakikisha Yanga inatinga robo fainali na pengine ilipaswa kuvuka hatua hiyo kama sio dhurma waliyofanyiwa Afrika Kusini katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Mamelodi Sundowns