Katika misimu hii miwili Azam Fc imeonekana kuwekeza nguvu kubwa kushindana na Yanga lakini mpaka sasa ni kama timu hiyo imebaki palepale
Msimu uliopita Azam Fc walikuja na mkakati wa 'kuibomoa Yanga' kwa kuwasajili wachezaji muhimu wa mabingwa hao wa Tanzania Bara
Walifanikiwa kumn'goa Feisal Salum mapema na baadae kuwasajili Yannick Bangala na Djuma Shabani ambaye hata hivyo waliachana nae pasipo kumtumia!
Msimu huu walianza kwa 'mbwembwe' wakiamini watakuwa washindani wa kweli wa Yanga katika mbio za ubingwa
Lakini mpaka wakati huu zikiwa zimesalia mechi nne tu ligi kufika tamati, Azam Fc wameachwa alama 11 na Yanga.Vita waliyonayo sasa ni kuwania nafasi ya pili ambayo pia hawana uhakika nayo
Pengine wanapaswa kurejea katika michoro yao kuandaa upya ramani yao ya vita kwani hilo 'dude' wanalojaribu kushindana nalo hawataliweza. Yanga ni lidude kubwa ambalo huwezi kushindana nalo labda liwe limelala
Ni kama Azam Fc wanajaribu kun'goa kisiki cha mpingo kwa kutumia panga wakati hata wale wenye shoka wameshndwa!
Katika misimu minne ambayo Simba walichukua ufalme wa soka la Tanzania, Yanga ilikuwa dhoofu baada ya Yusufu Manji aliyekuwa Mwenyekiti na Mfadhili wa klabu kuachia ngazi kutokana na kesi zilizokuwa zikimkabili
Lakini tangu GSM alipoingia na kutengeneza misingi mizuri ambayo imeifanya Yanga ijitegemee, ufalme wa soka la ndani umerejea kwa Wananchi na sasa chini ya Injinia Hersi Said, Yanga imeanza kuisaka heshima Kimataifa
Mataji 29 ya Ligi Kuu yako kibindoni, ni suala la muda tu Yanga itaandikisha taji la 30 msimu huu
Dalili zinaonekana Yanga itaendelea kushinda mataji msimu hadi msimu kwani ina viongozi bora, makini na sio watu wa propaganda