Mwishoni mwa msimu Yanga itaachana na mlinda lango Metacha Mnata ambaye mkataba wake utakuwa umemalizika
Tayari mabosi wa Yanga wameanza mchakato wa kusaka golikipa mwingine wa ndani ambapo jina la Amos Yona, mlinda lango wa Tanzania Prisons limetajwa
Yona amekuwa na msimu mzuri katika kikosi cha Tanzania Prisons kinachoshika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi
Yona akiwa chaguo namba moja Tanzania Prisons, amekusanya jumla ya 'cleansheet' nane msimu huu
Kinara wa 'cleansheet' ni Djigui Diarra wa Yanga ambaye anazo 13 akielekea kutwaa tuzo ya kipa bora kwa msimu wa tatu mfululizo
Yona atakuwa huru mwishoni mwa msimu kwani mkataba wake na Wajelajela hao utakuwa umemalizika
ADVERTISE HERE