Kabla ya Yanga kuikabili Kagera Sugar jana, maswali yalikuwa mengi kwa kiungo Mudathir Yahya kwa nini siku hizi hapigi simu?
Jibu la Mudathir lilikuwa moja tu, simu yake imeibiwa lakini yuko mbioni kuipata
Hatimaye jana imepatikana pale Azam Complex Mudathir akifunga bao pekee la ushindi wa Yanga katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar. Ni katika uleule muda ambao Mudathir ni hatari
Ilikuwa dakika ya 83 Mudathir aliweka mpira kambani akimalizia pasi ya Stephane Aziz Ki na kufunga bao lake la 9 msimu huu
Dakika ya 83 mpaka dakika ya 88 huu ndio muda wa Mudathir kupiga simu pale Azam Complex
Msimu huu amepiga simu mara nne katika muda huo na kuihakikishia Yanga alama 12 muhimu
Katika muda huo alifunga mabao ya ushindi katika mechi dhidi ya Namungo Fc, Dodoma Jiji, Mashujaa Fc na jana Kagera Sugar
Yanga inakaribia kutetea ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo baada ya ushindi dhidi ya Kagera Sugar
Alama 68 kileleni mwa msimamo wa ligi ikihitaji alama tano tu kati ya 12 (mechi nne) ili kurudisha ubingwa kabatini pale Jangwani
Kama Azam Fc na Simba zitatoshana nguvu katika mchezo utakaopigwa leo Wananchi wanaweza kuwa mabingwa May 13 kama watapata ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar mkoaani Morogoro