Klabu ya Yanga inatarajiwa kuachana na mlinda lango Metacha Mnata mwishoni mwa msimu, imefahamika
Metacha alijiunga na Yanga msimu uliopita katika usajili wa dirisha dogo akitokea klabu ya Singida FG kwa mkopo baada ya Aboutwalib Mshery kupata majeraha yaliyomuweka nje kwa muda mrefu
Baada ya Mshery kurejea katika utimamu wake, Metacha amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi kocha Miguel Gamondi akimtumia Mshery kama mbadala wa mlinda lango namba moja Djigui Diarra
Kuna uwezekano Metacha atarejea Singida lakini wakati huu akatua klabu ya Ihefu Fc (Singida Black Stars)
Yanga iko kwenye mchakato wa kusaka mlinda lango mwingine wa ndani
ADVERTISE HERE