FT : Yanga 1-1 Singida United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Apr 2018
FT : Yanga 1-1 Singida United
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Yanga wamelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Singida United kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Singida United ndio ilianza kuandika bao la kuongoza kwenye dakika ya tatu tu mfungaji akiwa Papi Kambale aliyeunganisha krosi ya Batambuze kutoka upande wa kushoto.

Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha Yanga ambayo baada ya mashambulizi kadhaa langoni kwa Singida United, ilifanikiwa kusawazisha kwenye dakika ya 45 mfungaji akiwa Abdallah Shaibu aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliokuwa umechongwa na Ajib.

Kipindi cha pili ni Yanga iliyotawala mchezo huo lakini washambuliaji wake walikosa umakini katika umaliziaji licha ya kufika mara kwa mara kwenye lango la Singida United.

Sare hiyo inaweza kuinufaisha Simba ambayo sasa inaongoza ligi kwa tofauti ya alama tano huku ikitarajiwa kucheza dhidi ya Mbeya City kesho.

Ushindi katika mchezo huo utaifanya ifikishe alama 55, na kuiacha Yanga kwa tofauti ya alama nane.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’