Baada ya kutoka kwa taarifa za kocha George Lwandamina kuwa amejiunga na Zesco uongozi wa Yanga umeitisha kikao cha dharura cha kamati ya utendaji leo jioni baada ya mchezo dhidi ya Singida United ili kujadili suala hilo.
Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Samuel Lukumay amesema wamelazimika kuitisha kikao hicho cha dharura kujadili kwa kina suala hilo ili lipatiwe ufumbuzi.
Lukumay alisema kikao hicho kitafanyika leo mara baada ya mchezo wao wa ligi kati ya Yanga na Singida United kikiitishwa na Kaimu Mwenyekiti Clement Sanga.
"Tumepokea hizo taarifa, lakini kwa sasa ni mapema kwa klabu kulitolea tamko ingawa nimepata taarifa hapa tutakuwa na kikao cha kamati ya utendaji leo usiku,"alisema Lukumay.
"Unajua mambo ni mengi, lakini kubwa tunataka tuwe na kauli moja kama klabu katika hili la kocha wetu kila mmoja wetu ameshtuka kusikia kocha ameondoka kwahiyo subirini mtapewa majibu."
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE