Kuna bango kubwa la utambulisho litakaa paleeee..

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 May 2024
Kuna bango kubwa la utambulisho litakaa paleeee..

Msimu huu Yanga imekuja na mtindo tofauti katika kunogesha utani dhidi ya wapinzani wao wa kihistoria, klabu ya Simba

Baada ya kuwanyoosha mabao 5-1 katika mchezo wa duru ya kwanza ligi kuu ya NBC, mabango yalitapakaa kila kona ya jiji la Dar es salaam na hata majiji mengine kama Mwanza, Arusha na visiwani Zanzibar

April 20 Yanga ikaongeza ushindi mwingine wa 2-1 katika mechi ya pili ya ligi msimu huu, Ali Kamwe akarejea tena kuwakera Simba kwa mabango ya 7-2 yaliyowekwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam

Sasa kuna kubwa zaidi linakuja! Mapema leo msemaji wa Yanga Ali Kamwe alidokeza kuwa kuna usajili wa mchezaji mmoja utambulisho wake utakuwa wa kihistoria

Nyota huyo atatambulishwa maeneo ya katikati ya jiji la Dar es salaam (Kariakoo) ambapo Yanga itakodisha eneo katika jengo linaloangaliana na jengo la klabu moja maarufu nchini na kisha kuweka bango lenye sura ya mchezaji huyo

Bango hilo litakaa katika eneo lake kwa miezi sita, kwa maana kila watakapokuwa katika jengo lao watakuwa wakisabahiana na picha ya aliyekuwa mchezaji wao!

Tetesi tayari zimeanza kuvuma huko mitaani, Kamwe amewaambia Wananchi 'wanywe mtori, nyama watazikuta chini...!'

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’