Yanga kuivaa Singida United bila Lwandamina

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Apr 2018
Yanga kuivaa Singida United bila Lwandamina
Mabingwa watetezi ligi kuu ya Vodacom Yanga leo wanashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Singida United bila ya uwepo wa kocha wake Mkuu George Lwandamina.

Jana klabu ya ZESCO United ilimtangaza Lwandamina kuwa kocha Mkuu wa timu hiyo akirithi mikoba ya Tenant Chembo aliyejiuzulu.

Lwandamina amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia ZESCO.

Mkataba wa Lwandamina na Yanga unamalizika mwishoni mwa mwezi Mei hata hivyo kocha huyo aliondoka kurejea kwao Zambia baada ya mchezo dhidi ya Wolaitta Dicha.

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga Salum Mkemi amethibitisha kuondoka kwa Lwandamina baada ya mchezo dhidi ya Dicha lakini juu ya kujiunga ZESCO amesema taarifa hizo wameziona kwenye mitandao ya kijamii.

Kocha Msaidizi Shedrack Nsajigwa anatarajiwa kukiongoza kikosi cha Yanga kuikabili Singida United inayonolewa na kocha wa zamani wa timu hiyo, Hans van Pluijm.

Yanga inahitaji kuibuka na ushindi ili kuweka hai matumaini ya kutetea ubingwa.

Kwa sasa iko nyuma ya Simba kwa tofauti ya alama sita, matokeo yoyote tofauti na ushindi huenda yakairahisishia Simba kutwaa ubingwa mapema.

Ukiacha mchezo huo, ligi kuu ya Vodacom inaingia kwenye mzunguuko wa 24 kwa michezo kadhaa kupigwa leo.

Michezo mingine inayopigwa leo;

Stand United vs Majimaji
Mbao FC vs Njombe Mji
Prisons vs Kagera Sugar
Mwadui vs Lipuli FC
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’