Yanga yaandaa hafla ya pongezi kwa Wazee

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 May 2024
Yanga yaandaa hafla ya pongezi kwa Wazee

Leo Makao Makuu ya klabu ya Yanga kulikuwa na tukio maalum lililoandaliwa na uongozi wa Yanga kwa ajili ya kuwashukuru na kuwapongeza Wazee wa klabu hiyo kwa kuhakikisha wametimiza vyema wajibu wao katika ile mechi ya dabi dhidi ya watani

Ni takribani siku 10 zimepita tangu Yanga iibuke na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba katika mchezo ambao Yanga iliwakabidhi Wazee 'Wazee Derby'

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema hafla hiyo ni maalum kwa ajili yao Wazee na uongozi unawapongeza, kutambua na kuthamini mchango wao

"Tumewaita wazee wetu leo kwa lengo la kuwashukuru lakini kuwaonyesha umuhimu wenu kwa Klabu hii. Tumekuwa na kawaida ya kuwaita tunapotafuta ushindi, hatuwezi kuwasahau pale ambapo ushindi umepatikana. Tukiachana na ushindi lakini tunaamini pia sisi kama vijana tunahitaji hekima zenu wazee. Nyie ndio nguzo iliyoshikilia maendeleo ya Klabu hii," alisema Arafat

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said aliwashukuru Wazee kwa kuendelea kuwa bega kwa bega na uongozi wake na kuitikia wito pale walipohitajika

Hersi alitoa zawadi kwa wazee hao pia akiwapa ofa ya kushuhudia mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Tabora United utakaopigwa usiku wa leo katika uwanja wa Azam Complex

Wazee wameandaliwa usafiri wa kuwapeleka Azam Complex na kuwarudisha baada ya mchezo huo ambao Yanga inasaka tiketi ya kutinga nusu fainali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’