Taarifa ya kocha wa Yanga George Lwandamina kurejea ZESCO United imethibitishwa leo na timu hiyo mbele ya vyombo vya habari nchini Zambia.
Lwandamina amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia ZESCO
Tulibahatika kupata taarifa za Lwandamina kutakiwa na timu hiyo mwezi uliopita, japo mwanzoni taarifa hizo zilikanushwa na pande zote, lakini tayari Lwandamina anarejea ZESCO.
Yanga imekumbwa na changamoto nyingi sana msimu huu, hata hivyo Lwandamina anastahili pongezi kwa juhudi zake za kuijenga Yanga upya.
Sasa tunaishuhudia Yanga yenye idadi kubwa ya wachezaji vijana ambao kama wataendelezwa wataifanya Yanga iwe moto wa kuotea mbali msimu ujao.
Ni swala la muda tu Yanga italazimika kusaka mbadala wa kocha huyo.
Mkataba wa Lwandamina unamalizika mwishoni mwa msimu, lakini kama ZESCO imemtangaza rasmi huenda akaondoka mapema zaidi

ADVERTISE HERE