Ukijichanganya 5G ya Yanga inakuhusu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Apr 2024
Ukijichanganya 5G ya Yanga inakuhusu

Mkufunzi wa Yanga Miguel Gamondi amesema katika kila mechi huandaa timu yake kwa ajili ya kupigania alama tatu bila ya kujali idadi ya mabao ambayo watafunga

Kocha huyo kutoka Argentina amebainisha kuwa hakuna mechi walipanga kushinda mabao matano lakini walifunga idadi hiyo ya mabao kutokana na makosa yaliyofanywa na wapinzani wao

Gamondi alitoa kauli hiyo juzi baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0

Katika mchezo huo Yanga ilitengeneza nafasi nyingi lakini wananchi walitumia nafasi moja tu kupitia kwa Joseph Guede

"Hatujawahi kutoka kambini tukasema tunakwenda kuwafunga wapinzani mabao matano, kushinda mabao mengi inategemea na makosa gani mpinzani ameyafanya dhidi yetu"

"Tuna staili ya soka letu namna ya kutafuta ushindi, kitu muhimu kwetu ni kushinda kwa kupata pointi tatu na kucheza soka la kuvutia"

"Angalia mechi dhidi ya Coastal Union, ingewezekana kushinda mabao mengi, wapinzani wetu walijua wanakuja kukutana na timu gani wakaamua wote kucheza nyuma ya mpira bado haikuwa shida tulitawala mchezo na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga"

"Bahati yao ni kwamba langoni walikuwa na kipa mzuri ambaye sio vibaya tukimpongeza kwa kufanya kazi kubwa, kinyume cha hapo tungeweza pia kutengeneza ushindi mkubwa, kitu muhimu malengo yetu ni kushinda na tumefanikiwa," alisema Gamondi

Kikosi cha Yanga kimerejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Tabora United utakaopigwa Jumatano, May 01 katika uwanja wa Azam Complex

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
26m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’