Huyu Lwandamina ni bonge la kocha, Yanga imbakishe kwa gharama yoyote

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
10 Apr 2018
Huyu Lwandamina ni bonge la kocha, Yanga imbakishe kwa gharama yoyote
Kumekuwa na sintofahamu juu ya hatma ya kocha wa Yanga George Lwandamina ambaye anahusishwa na kurejea ZESCO United mwishoni mwa msimu.

Lwandamina alijiunga na Yanga mwezi Novemba mwaka 2016 kuchukua nafasi ya Hans van Pulijm ambaye alipandishwa cheo na kuwa Mkurugenzi wa ufundi.

Hata hivyo baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji kupata matatizo na kuamua kujiweka pembeni, mambo yalianza kwenda kombo katika klabu ya Yanga.

Ilipelekea Yanga kufuta cheo cha Ukurugenzi wa Ufundi na kuachana na Pluijm ambaye alienda kujiunga na Singida United.

Licha ya changamoto nyingi katika msimu wake wa kwanza, Lwandamina alifanikiwa kutetea ubingwa wa VPL kwa msimu wa tatu.

Yeye alimalizia nusu ya pili ya msimu huo kwani nusu ya kwanza ilikamilishwa na Pluijm.

Kwa Lwandamina msimu wa 2017/18 ndio msimu wake kamili wa kwanza. Nao haujawa mzuri kwani changamoto alizomaliza nazo msimu wa 2016/17 alianza nazo msimu huu.

Changamoto zaidi ziliongezeka kama majeruhi, migomo ya hapa na pale ya wachezaji wakidai maslahi.

Kuna wakati Yanga ilikuwa na wachezaji 11 majeruhi na wengi tulipoteza matumaini kuwa haupo uwezekano wa Yanga kufanya chochote msimu huu.

Hata hivyo mpaka sasa Lwandamina amedhihirisha kuwa yeye ni miongoni mwa makocha bora watakaobaki kwenye kumbukumbu za Yanga pale atakapoondoka.

Ameweza kutengeneza kikosi imara kwa kutumia wachezaji alionao. Amewapa moyo wachezaji pale wanapokuwa katika mazingira magumu.

Kuna watu hawaamini Yanga hii ya msimu huu imewezaje kuwa hapo ilipo. Hata Simba iliyokuwa inaamini itatwaa ubingwa kwa urahisi sasa wameingia mchecheto.

Siri ya mafanikio haya ni ubunifu wa kocha, uvumilivu na usikivu wake. Lwandamina amekuwa akiwajali wachezaji wake pengine kuliko yeye mwenyewe.

Kuna wakati ilielezwa kuwa kocha huyo aligoma kupokea mshahara wake kwa kutaka walipwe kwanza wachezaji. Ni nadra sana kumpata kocha wa aina hii.

Naamini Yanga bado ina nafasi ya kumbakisha pale mkataba wake utakapomaliza mwezi ujao.

Mwenyewe ameonyesha anaipenda Yanga na amekuwa akifanya kazi katika mazingira magumu.

Ikumbukwe Yanga iko mbioni kufanya mabadiliko mwezi ujao.

Mabadiliko ambayo huenda yakamaliza kabisa matatizo ya kiuchumi yanayoisumbua klabu mara kwa mara.

Utegemezi wa wafadhili umeigharimu Yanga kwa miaka mingi, mwaka huu imepata funzo na hakika mabadiliko limekuwa swala la lazima.

Lwandamina tayari ametengeneza msingi mzuri, naamini akiendelea kubaki Yanga atatengeneza timu inayoweza kutwaa hata ubingwa wa Afrika.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’