Yanga Princess itaendelea kuimarishwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Apr 2024
Yanga Princess itaendelea kuimarishwa

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema uongozi utaendelea kuiboresha timu ya Wanawake ya Yanga Princess ili kuwa miongoni mwa timu bora katika ligi ya Wanawake nchini

Arafat amesema timu hiyo imekuwa katika maboresho katika hii misimu miwili lakini anatambua bado timu haijafika katika ubora inayopaswa kuwa

Arafat amewashukuru wale wanaotoa maoni yao lakini pia hata wale wanaokosoa kwani lengo ni moja kuifanya timu hiyo iendane na ukubwa/heshima ya klabu ya Yanga

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Arafat amewapa Wananchi ujumbe huu;

Dhumuni langu kubwa kama Makamu wa Rais wa Young Africans kulihodhi jukumu la soka la Wanawake ni kwa mantiki mbili kubwa, kwanza kama Kiongozi nia ni kuona timu zetu zote zinafanya vyema kama ambavyo tuliahidi wakati tunaomba ridhaa na pili ni Baba mwenye Binti pia, jukumu la pili kama Mzazi ni kuona Mabinti wanafanikiwa,hizi zote ni ndoto zangu na naamini zitafanikiwa.

Nimeona maoni mengi, machapisho mengi na niseme wazi ni furaha yangu kubwa kwakuwa kichwa kizito ndicho huvaa kofia ya Kifalme, hii ina maana kuwa soka la Wanawake limepiga hatua kubwa na linafuatiliwa na ni wazi WANANCHI wanataka matokeo mazuri kutoka kwenye timu yao, nimefurahishwa na hili kutokana na hili kuonesha hamu ya mafanikio ndio mafuta ya kuchochea Project hii adhimu.

WANANCHI msimu huu tumeingia na kikosi chenye thamani na maingizo mapya ya Wachezaji 12 wa Kimataifa, ambao wana profile nzuri mno lakini mpira wa miguu hukupa matokeo tofauti na matarajio, PROJECT THE PRINCESS inahitaji muda ili ikomae hata timu ambazo zipo imara zilitumia muda kujijenga, nafahamu uzito wa jezi hii na Wachezaji wanafahamu hilo, lakini Roma haikujengwa kwa siku moja.

Bado naendelea na PROJECT hii, nafurahi kuona nikikosolewa na nafurahi zaidi kwakuwa sote tupo kwenye kujenga ila tufahamu Project hii sio push to start, kwenye safari tutakuwa na β€˜trial and errors’ ila tunaenda huku na kesho yetu ni njema sana, asanteni WANANCHI kwa support kubwa tuendelee kuwaamini Mabinti zetu na wakati utaongea, PROJECT THE PRINCESS in the making.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’