Licha ya jitihada zinazofanyika kutoka kwa vilabu na hata TFF katika kupandisha hadhi ya ligi, kuruhusu mechi kuchezwa katika mazingira ya viwanja visivyo na hadhi ni kusaliti jitihada hizo
Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga Simon Patrick ameeleza masikitiko yake baada ya mchezo kati ya JKT Tanzania dhidi ya Yanga uliopigwa uwanja wa Meja Jen Isamuhyo na kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
"Mpira wa miguu ni biashara na burudani kwa watazamaji, kuna namna vilabu vinapambana kupandisha hadhi ya ligi mpaka kufika kuwa ligi ya tano kwa ubora Afrika"
"Lakini wasimamizi ligi yetu na wao kuna muda wanakuwa na mtazamo na malengo tofauti"
"Kwa watu wanaojua umuhimu wa 'brand' wasingeruhusu mchezo wa ligi kuu inayofatiliwa na mataifa mbali mbali kwa sasa ichezeke kwenye tope kama lile"
"Natambua uhaba wa miundo mbinu ya viwanja Tanzania ila siamini kama tungekua serious na brand ya ligi yetu tungekosa uwanja mbadala"
"Yote kwa yote niwapongeze Yanga kwa matokeo haya, kupata matokeo ya namna hii kama haujui kuogelea na kuteleza kwenye tope ni ngumu sana," aliandika Simon katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii