Mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya JKT Tanzania dhidi ya Yanga uliopigwa uwanja wa Meja Jen Isamuhyo umemalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Mchezo huo awali ulipangwa kupigwa jana lakini uliahirishwa kutokana na uwanja wa Isamuhyo kujaa maji
Bado mazingira ya uwanja wa huo hayakuruhusu mpira kuchezwa haitakuwa ajabu uwanja huo ukafungiwa baada ya mchezo wa leo
Ni wazi ilikuwa ni lazima Yanga wacheze katika uwanja huo bila ya kujali ubora wake kwa kuwa tu, mtani wake alicheza
Alama moja kwa Wananchi si haba, alama 59 kileleni mwa msimamo wa ligi
ADVERTISE HERE