Yanga leo ilikuwa tayari kuikabili JKT Tanzania katika mchezo wa ligi kuu uliopaswa kupigwa uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni jijini Dar es salaam
Hata hivyo mchezo huo haukufanyika kutokana na uwanja kujaa maji
Wananchi wanasubiri taarifa ya Bodi ya ligi kufahamu mchezo huo utapigwa lini
"Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya JKT Tanzania na Yanga uliokuwa uchezwe leo kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, umeahirishwa kwa mujibu wa Kanuni ya 39:13 ya Ligi Kuu kuhusu Mwamuzi na Bodi itatoa taarifa ya ratiba ya mchezo huo," ilisema taarifa ya Bodi









ADVERTISE HERE