Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema mlinzi Joyce Lomalisa hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili JKT Tanzania hapo kesho katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa uwanja wa Meja Jen. Isamuhyo jijini Dar es salaam
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa habari mapema leo, Gamondi alisema Lomalisa alipata majeraha ya misuli katika mchezo uliopita dhidi ya Simba
Aidha Gamondi amebainisha kuwa kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua bado anaendelea na program maalum ya 'recovery' hivyo hatakuwa tayari kutumika hapo kesho
"Lomalisa amepata matatizo ya misuli ya paja, madaktari wameniamba sio jereha kubwa sana lakini nadhani tutahitaji kumuangalia tutakaporejea mazoezini leo"
"Pacome bado anaendelea na program maalum, natarajia wiki hii atakuwa na mazoezi zaidi ya fitness hivyo sidhani kama atakuwa tayari kutumika, tutaangalia kwa mechi zitakazofuata," alisema Gamondi

Akizungumzia mchezo dhidi ya JKT Tanzania, Gamondi anasema anafahamu ni timu ngumu inaweza kuzuia kutokea chini 'low block'
"Nafahamu katika mechi tano zilizopita, wamepoteza mchezo mmoja na kutoka sare michezo minne, wanazuia katika 'low block'. Tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini tumejiandaa kukabiliana nao"
Katika mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-0