Klabu ya Yanga na Simba ndio zilipaswa kushiriki michuano ya Muungano kwa upande wa Tanzania Bara baada ya kumaliza nafasi ya kwanza na ya pili ligi kuu ya NBC msimu uliopita
Hata hivyo Yanga iliomba kutoshiriki michuano hiyo hivyo nafasi yao kupewa Azam Fc
Imeelezwa sababu walizotoa Yanga zilikuwa na mashiko ndio maana mabingwa hao wa Tanzania Bara ombi lao la kutoshiriki likakubaliwa
Yanga imetoka kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ikifanikiwa kufika robo fainali. Kuna mechi mbili za viporo ligi kuu na huku Wananchi pia wakikabiliwa na mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la CRDB mwanzoni mwa May 2024
Ni tofauti na watani zao Simba ambao kwa sasa hawana mashindano mengine ambayo wanashiriki baada ya kuwa wameondoshwa katika michuano yote, wakibaki na ligi kuu pekee
Aidha hata Azam Fc hawakucheza mechi nyingi msimu huu kulinganisha na Yanga, kwenye ligi hawana viporo wakiwa wamecheza mechi 24
Lakini pia michuano hii ni kama imekuja 'ghafla', bila shaka TFF na ZFF wataiingiza katika kalenda msimu ujao kama walivyofanya kwa kombe la Mapinduzi
Msimu ujao michuano hiyo inatarajiwa kushirikisha timu nane, nne kutoka Bara na nne kutoka Visiwani Zanzibar