Baada ya kukamilisha mpango wa kumpiga mtani nje..ndani, kikosi cha Yanga sasa kinaelekeza nguvu katika kukamilisha mechi zilizosalia kutetea ubingwa wa ligi kuu ya NBC kwa msimu wa tatu mfululizo
Kesho Jumanne, April 23 Yanga itakuwa dimba la Meja Jenerali Isamuhyo kuikabili JKT Tanzania katika mchezo wa raundi ya 23 ambao ni kiporo
Ni mchezo mwingine muhimu kwa Yanga kushinda ili kufunga hesabu mapema
Yanga imebaki na mechi nane lakini kimahesabu Wananchi wanahitaji kushinda mechi tano tu ili kuwa mabingwa
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema shamra-shamra za 'kumkanda' mtani zimemalizika na sasa wanaelekeza nguvu katika mchezo unaofuata
ADVERTISE HERE