Bao alilofunga Aziz Ki jana katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba lilikuwa la 15 na hivyo kumfanya aendelee kujiimarisha katika mbio za ufungaji bora
Aziz sasa amefunga mabao mawili zaidi ya Feisal Salum wa Azam Fc mwenye mabao 13 huku Yanga ikiwa bado ina mechi moja ya kiporo
Katika mechi nane zilizosalia Aziz Ki anahitaji kufunga angalau mabao mawili ili kuvunja rekodi ya mabao 16 ya Fiston Mayele ambaye kwa sasa ni mdomo unaofanya kazi zaidi kuliko miguu yake
Aziz Ki amekuwa na msimu bora chini ya Kocha Miguel Gamondi pengine kuliko wakati mwingine wowote katika maisha yake ya soka
Kuna kila dalili ataibuka mfungaji bora huku pia akiwa bao moja tu nyuma ya kinara wa pasi za mabao, Ki ana assist 7
ADVERTISE HERE