Habari ndio hiyo, Wananchi wamefanikiwa kuchukua alama nyingine tatu mbele ya Simba kwa ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga ilihitaji dakika 45 za kipindi cha kwanza kufunga mabao yake kupitia kwa Stephane Aziz Ki na Joseph Guede aliyefunga moja ya mabao bora msimu huu
Aziz Ki alifunga bao la uongozi katika dakika ya 20 kwa mkwaju wa penati baada ya kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari
Aziz Ki alifanya pressing na kufanikiwa kumnyan'ganya mpira mlinzi wa Simba Hussein Kazi ambaye alimuangusha ndani ya eneo la hatari
Baada ya kufunga bao hilo, Yanga iliendelea kulishambulia lango la Simba na Guede akafunga bao la pili dakika ya 38 akikimbia nyuma ya migongo ya walinzi wa Simba na kupokea pasi ya Khalid Aucho
Kipindi cha pili Yanga ilipunguza kasi na kuwapa Simba nafasi ya kushambulia na kufanikiwa kufunga bao la kufutia machozi kupitia Fred Michael
Ni alama tatu muhimu kwa Yanga ambazo sasa zinawaweka Wananchi katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa
Master Miguel Gamondi amerudia kile kilichowahi kufanywa na Hans Van Pluijm kwa kushinda nje ndani dhidi ya Simba