Klabu ya Yanga huenda isitumie vyumba vya kubadilishia nguo katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa kuanzia saa 11 jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga ni kuwa kuna harufu kali ya dawa katika chumba ambacho Yanga wanapaswa kutumia leo
Uongozi umewasilisha malalamiko kwa msimamizi wa mchezo na amethibitisha malalamiko hayo hivyo huenda Yanga ikaruhusiwa kutotumia vyumba
Ifahamike pamoja na kuwa Yanga ni mwenyeji wa mchezo huu lakini sio jukumu lao kusimamia uwanja huo unaomilikiwa Serikali
ADVERTISE HERE