Baraza la Wazee wa Yanga wamesema wanamtakia mafanikio mema kiungo wake, mshambuliaji Simon Msuva anayetarajia kujiunga na Klabu ya Difaa Hassani El Jadidi inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco.
Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali amesema kuwa kwa upande wao wanatoa baraka zote kwa mchezaji huyo ili aweze kufanikiwa zaidi baada ya kuitumikia Yanga kwa mafanikio makubwa.
"Leo (jana) tulikuwa na kikao cha Baraza la Wazee wa Yanga na kikubwa ilikuwa ni kujadili suala la kijana wetu Msuva ambaye ameuzwa kwenda kucheza soka Morocco, wazee wa Yanga kwa upande wetu tumeridhia kuondoka kwake.
"Unajua kwa upande wetu ni heshima kubwa kwa klabu yetu kufungua milango ili vijana wetu waweze kucheza soka la kulipwa na ni heshima kubwa, mafanikio aliyotuachia ni makubwa na tunayaheshimu kwa sababu siku akiamua kurejea kucheza hapa atarudi kwenye timu yake ambayo imemkuza na kumpa mafanikio," alisema Akilimali.

ADVERTISE HERE