Yanga ni mbabe wa derby za Jumamosi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Apr 2024
Yanga ni mbabe wa derby za Jumamosi

Mashabiki wa Yanga na Simba tayari viroho vimeanza kuwadunda, wakati timu zao leo zikitarajiwa kuchuana katika pambano la Ligi Kuu Bara litakalopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Yanga inaingia katika mchezo huo ikiwa na morali kubwa hasa baada ya mechi yao ya mwisho iliyopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Novemba 5, 2023 kuifunga Simba kwa mabao 5-1.

Katika mchezo huo wa mwisho mabao ya Yanga yalifungwa na Maxi Nzengeli aliyefunga mawili wakati Kennedy Musonda, Pacome Zouzoua na Stephane Aziz KI wakifunga moja kila mmoja wao huku la Simba la kufutia machozi likifungwa na Kibu Denis.

Rekodi zinaonyesha timu hizo zimekutana mara 60 Jumamosi katika Ligi Kuu Bara tangu zilipoanza kukutana mwaka 1965 huku Yanga ikiwa mbabe zaidi mbele ya Simba kwani imeshinda mara 25 na kupoteza 16 huku michezo 19 ikienda sare

Katika michezo hiyo, yamefungwa jumla ya mabao 124 na Yanga imefunga 72 huku kwa upande wa watani zao Simba ikifunga 52.

Kichapo kikubwa kinachokumbukwa Jumamosi ni kile Yanga ilichoifunga Simba wakati ikifahamika kama Sunderland cha mabao 5-0, Juni 1, 1968 yaliyofungwa na Maulid Dilunga na Salehe Zimbwe waliofunga mawili kila mmoja na Kitwana Manara.

Hata hivyo hili ni pambano la 14 kwa timu hizo kukutana Aprili katika Ligi Kuu Bara tangu 1965 na katika mechi 13 zilizopita Simba imeshinda minne huku Yanga ikishinda mara tatu na michezo mingine sita iliyobakia ilimalizika sare

Kocha wa zamani wa Yanga na Singida Fountain Gate, Hans Van de Pluijm alisema mchezo baina ya miamba hiyo siku zote huwa hautabiriki kutokana na ugumu wake kwa sababu mtu mmoja anaweza kufanya jambo linaloweza kuleta faida au hasara kwenye timu.

"Huwa ni mchezo mkubwa na mgumu kwa kila timu ingawa ukiangalia kwa mwenendo wa Yanga kwa sasa unaweza kuipa ushindi japo ninachoamini atakayekuwa makini kwenye kutumia vizuri nafasi na kuepuka makosa ndiye atakayekuwa na faida zaidi," alisema

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’