Yanga iko tayari, kukamilisha maandalizi leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Apr 2024
Yanga iko tayari, kukamilisha maandalizi leo

Kikosi cha Yanga kimekuwa na siku nne za maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Unaweza kusema siku ya kesho ndio ile siku ya kukata mzizi wa fitina na kumaliza tambo za takribani wiki nzima

Yanga wakiwa vinara wa ligi kuu wanafahamu ushindi dhidi ya watani zao Simba utawasogeza karibu na ubingwa wa 30

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ataingia katika mchezo huo akiwa na kikosi chake kamili, ni jukumu lake kuamua nani amtumie katika mchezo huo

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi katika siku hizi nne zilizopita na pengine baada ya mazoezi ya mwisho leo, Gamondi atafahamu nyota wake 20 atakaowapa jukumu la kuilinda heshima ya Yanga pale dimba la Mkapa

Pamoja na kupata ushindi mnono wa mabao 5-1 katika mchezo wa kwanza, Yanga imechukua tahadhari kubwa kuelekea mchezo huo

Mechi ya dabi ya Kariakoo ndio mechi kubwa zaidi ya soka Tanzania, wakati mwingine mechi hii hukumbwa na mambo mengi yakiwemo masuala ya nje ya uwanja

Ndio maana viongozi wamechukua tahadhari kubwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi pale Avic Town

Zitakuwa dakika 90 ngumu lakini jambo la uhakika ni kuwa Gamondi amekiandaa kikosi chake kwa ajili ya kupambana na kupata ushindi siku ya Jumamosi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’