Dicha wamvulia kofia Ninja

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
10 Apr 2018
Dicha wamvulia kofia Ninja
Habari ya Yanga kumkosa beki wake, Kelvin Yondani kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, ilishtua mashabiki wa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, lakini kocha George Lwandamina, akawashusha presha.

Lwandamina alimwangalia kwa makini beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ kisha akasema huyu ataziba pengo la Yondani na kuanza kumfua na juzi Jumamosi, Ninja akathibitisha si mtu wa kuchezea pale aliposhirikiana na Andrew Vincent ‘Dante’ kuweka ukuta wa maana.

Hiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza ya kimataifa kwa Ninja tangu asajiliwe kutoka Taifa Jang'ombe ya Zanzibar.

Sasa yule straika matata wa Welaytta Dicha, Mtogo Arafat Djako amempigia saluti kwa kusema jamaa ni bonge la beki.

“Yanga wamecheza vizuri sana hasa sehemu ya beki na winga. Mchezaji ambaye alitupa wakati mgumu ni yule beki wa kati mrefu si yule mwenye rasta ni yule namba 6 nafikiri (Ninja). Alicheza vizuri na amechangia kuharibu mipango yetu,” alisema Djako.

wa upande wa beki wa kati wa Welaytta, Bzabih Melayu alisema: “Yanga ni wazuri hivyo tunakwenda kujifua ili kuhakikisha hatufanyi makosa, kwetu tutawafunga kwetu bila wasiwasi.”

Katika mchezo huo, Yanga walishinda mabao 2-0 na watacheza tena mechi ya maruadiano nchini Ethiopia Aprili 18.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE →