Pacome arejea, Gamondi kuamua Jumamosi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Apr 2024
Pacome arejea, Gamondi kuamua Jumamosi

Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua, ameanza mazoezi ya ushindani na wachezaji wenzake baada ya kukaa nje ya uwanja kwa siku 29 akiuguza jeraha la nyama za paja

Yanga itaikaribisha Simba kwenye Derby ya Kariakoo, Jumamosi April 20 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, ikiwa ni mechi ya raundi ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara

Nyota huyo raia wa Ivory Coast, aliumia katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC, uliochezwa March 17, mwaka huu, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam

Daktari wa Yanga, Moses Etutu amethibitisha kuwa Pacome ameanza mazoezi ya ushindani na wachezaji wenzake baaada ya kukamilisha program binafsi ya mazoezi

Hata hivyo Etutu amesema hatma ya mchezaji huyo kutumika katika mchezo dhidi ya Simba Jumamos itategemea na utayari wake na mpango wa Kocha Miguel Gamondi

"Pacome tayari ameanza mazoezi na wenzake, kuhusu kumtumia katika mchezo ijao hiyo ni kazi ya benchi la ufundi, kumpa nafasi au kuendelea kumsubiri na kumpa dakika chache za kucheza kwa ajili ya kuwa fiti zaidi," alisema Etutu

Pacome alikosa mechi nne za Yanga ikiwemo mechi mbili za ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns kutokana na majeraha hayo ambayo awali yalionekana yasingemuweka nje kwa muda mrefu

Nyota wengine ambao walikuwa majeruhi na tayari wamerejea kikosini ni Khalid Aucho, Kibwana Shomari, Zawadi Mauya na Yao Kouassi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’