Ushindi dhidi ya Singida United ni muhimu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Apr 2018
Ushindi dhidi ya Singida United ni muhimu
Keshokutwa Jumatano April 11 2018 Yanga itashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabiki Singida United kwenye moja ya michezo ya kuamua hatma ya ubingwa kwa Yanga.

Yanga inakumbana na Singida United kwa mara nyingine ikiwa ni baada ya siku nane kupita tangu wababe hao wa soka la Tanzania kuondoshwa katika hatua ya robo fainali ya kombe la FA na hao hao Singida United mkoani Singida.

Yanga itashuka uwanjani kulipa kisasi baada ya kipigo kile cha mikwaju ya penati.

Lakini pia Yanga inalazimika kushinda mchezo huo ili iendelee kuweka hai matumaini ya kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo.

Baada ya mchezo dhidi ya Singida United, Yanga haitakuwa na mchezo wowote wa ligi hadi baada ya kucheza na Wolaitta Dicha mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho April 18.

Wakati Yanga ikitekeleza majukumu ya Kimataifa, Simba itacheza michezo miwili hadi mitatu zaidi kabla timu hizo hazijakutana kwenye mchezo baina yao April 29.

Ushindi dhidi ya Singida United utaifanya Yanga irejeshe tofauti ya pointi baina yake na Simba kuwa tatu baada ya Simba leo kuifunga Mtibwa Sugar 1-0 na kufikisha alama 52.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’