Mpaka sasa tiketi za VIP A zimemalizika, mashabiki wa Yanga wameaswa kuendelea kununua tiketi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi April 20 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 11 jioni
Yanga ndio mwenyeji wa mchezo huo hivyo wingi wa mashabiki utaongeza hamasa ya wachezaji wao katika mtanange huo ambao Wananchi wanahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wa ligi kuu
Ukiwasikiliza mashabiki wengi wa Simba wanadai hawatakwenda uwanjani lakini hii inaweza kuwa propaganda tu ili kuwaaminisha Yanga kuwa mchezo huu tayari wameshinda
Lakini kiuhalisia mchezo utakuwa mgumu na wengi watakuwepo uwanjani. Itakuwa aibu kwa Yanga kama mashabiki hawatajitokeza kwa wingi kwani kwa sasa Yanga ndio timu bora Tanzania yenye uhakika wa kuwapa furaha mashabiki wake katika kila mechi