Kazi kwenu Mzee Mpili na wenzako

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Apr 2024
Kazi kwenu Mzee Mpili na wenzako

Katika Mkutano na Wanahabari jana, Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe alitangaza kuwa wamewakabidhi Wazee mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi, April 20 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Kwa wale waliosoma Cuba nafikiri walielewa alimaanisha nini! Wakati huu Wananchi hawataki yale ya msimu uliopita yajirudie

Ilikuwa April 16 siku kama ya leo pale uwanja wa Benjamin Mkapa Yanga wakati huo ikinolewa na Kocha Nasreddine Nabi ilipoteza alama zote mbele ya Simba kwa kufungwa mabao 2-0

Ni Yanga iliyokuwa bora kwelikweli, iliyokuwa ikifunga kila timu katika michuano ya kombe la Shirikisho ambayo Wananchi waliweza kufika fainali

Lakini mambo yalikuwa tofauti katika mchezo huo, wachezaji walikuwa wazito na hata wao hawakuelewa nini kilitokea

Wapo wanaoamini kuwa Wazee wa upande wa pili walifanya kazi yao vyema kwani siku ya mechi tangu asubuhi ilipiga mvua mwanzo mwisho

Wakati huu Yanga haitaki yajirudie ya msimu uliopita. Licha ya kushinda mabao 5-1 katika mchezo wa duru ya kwanza, Wananchi wanafahamu mechi ya April 20 ni mechi mpya na itakuwa ngumu

Lazima maandalizi kabambe yafanyike pale Avic Town lakini pia ni lazima Wazee waingie kazini kupambana na Wazee wenzao wa upande wa pili

Haya Mzee Mpili na wenzako mpira umeletwa mikononi mwenu...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’