Yanga, NBC Bank kushirikiana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Apr 2024
Yanga, NBC Bank kushirikiana

Klabu ya Yanga leo imeingia makubaliano ya ushirikiano na Bank ya NBC ambapo kupitia ushirikiano huo, Wanachama na Mashabiki wa Yanga wanaweza kujisajili na kulipa ada za uanachama katika benki ya NBC. Ni ushirikiano ambao Yanga pia imeingia na mabenki mengine kama CRDB na NMB

Akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano hayo iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es salaam mapema leo, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alisema Yanga inajivunia kuingia katika makubaliano hayo ambayo yatarahisisha kuwahudumia Wanachama kwenye Usajili na kutoa Kadi za Uanachama

"Ukijiunga kuwa Mwanachama wa Yanga, kupitia Benki ya NBC utapata kadi ya Uanachama na hapo hapo utapata huduma za kibenki, Lakini kubwa zaidi kadi ya NBC imeunganishwa na huduma za N CARD hivyo Mwanachama wetu atapata huduma ya kuingia Uwanjani pamoja na huduma za Usafiri"

"Niwaombe pia Benki ya NBC kutazama fursa nyingi zilizopo ndani ya Klabu yetu tuna Wanachama ndani na nje ya nchi na tunaamini Yanga ndio Klabu sahihi ya kufanya nayo kazi kwenye sekta ya michezo na nyie ni mashahidi, tangu mdhamini Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Bingwa ni Yanga na niwahakikishie, kama mtaongeza Mkataba wa miaka 10 mbele, Bado Yanga atabaki kuwa Bingwa katika kipindi chote hiko," alisema Hersi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’