Pacome, Yao waendelea kuimarika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Apr 2024
Pacome, Yao waendelea kuimarika

Wachezaji Pacome Zouzoua na Yao Kouassi wameendelea kuimarika na pengine Wananchi watarajie kuwaona uwanjani hivi karibuni

Pacome na Yao ndio wachezaji pekee ambao bado ni majeruhi baada ya Kibwana Shomari na Khalid Aucho kurejea dimbani na kutumika kwa dakika chache katika mchezo uliopita wa kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Dodoma Jiji

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wachezaji hao wameendelea na program zao maalum kuwaimarisha kabla ya kurejea uwanjani

"Taarifa za wachezaji wetu majeruhi Yao Kouassi na Pacome Zouzoua ni kuwa wanaendelea vizuri"

"Juzi tumemshuhudia Aucho akirejea uwanjani baada ya kupona majeraha tutarajie hawa wengine nao kuwaona uwanjani karibuni," alisema Kamwe

Yanga inatarajiwa kusafiri kuelekea mkoani Mwanza leo kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida FG utakaopigwa Jumapili, April 14 katika uwanja wa CCM Kirumba

Wananchi huenda wakamshuhudia Pacome akirejea katika mchezo huo huku Yao akiendelea kuandaliwa kwa ajili ya kuikabili Simba, April 20

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’