Uongozi wa Yanga chini ya Rais Injinia Hersi Said umepuuza tuhuma na kashfa alizotoa aliyewahi kuwa mshambuliaji wao Fiston Mayele
Juzi Azam TV walirusha mahojiano baina yao na mshambuliaji huyo ambapo aliendelea na mashambulizi yake dhidi ya waajiri wake hao wa zamani
Hata hivyo busara ikawaongoza Azam Tv, jana wakafuta video za mahojiano hayo katika kurasa zao za mitandao ya kijamii na Youtube
Ukweli ni kuwa Mayele amepoteza hadhi ya kujibiwa na klabu ya Yanga kwani amedhihirisha pengine hata nafasi aliyopata kuitumikia Yanga ilikuwa bahati tu
Ikumbukwe wakati Simba iko Misri kucheza na Al Ahly Mayele alionekana katika kambi ya klabu hiyo akiwa na viongozi wa Simba na inaaminika hata mahojiano hayo yalirekodiwa huko
Ni mchezaji ambaye amekubali kutumika kuichafua timu ambayo imempa heshima kubwa ya kutambulika barani Afrika. Hiki anachofanya kitammaliza yeye mwenyewe kwani anapoteza uaminifu
Kwa wale wanaomtumia wanapaswa kufahamu Yanga ilishatoka huko kwenye propaganda. Njia pekee ya kushindana na Yanga ni uwanjani
Uongozi wa Yanga umewekeza kwenye mpira zaidi, matunda ya uwekezaji huo ndio yanayowatesa wapinzani wao sasa wakijaribu kutumia kila mbinu kuishusha brand ya Yanga
Azam TV kama washiriki wa kibiashara wa Yanga walitaka kunasa katika mtego ambao hata hivyo baadae waliung'amua na kuamua kukataa kuwa sehemu ya propaganda chafu zinazofanywa dhidi ya Yanga
Hili ni tukio ambalo lingeweza kuathiri mahusiano ya kibiashara kati ya Yanga na Azam Media