Kiungo Thabani Kamusoko amewashukuru mashabiki wa Yanga kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa kwanza wa mtoano kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Wolaitta Dicha jana.
Kamusoko amesema mchezo wa jana ulikuwa mzuri kwa upande wao na wana matumaini makubwa ya kutinga hatua ya makundi kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu.
"Tunashukuru mashabiki kwa kutuunga mkono kwenye mchezo wa jana. Mchezo ulikuwa mzuri, sasa tuna matumaini ya kutinga hatua ya makundi kwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu."
"Ahsanteni sana kwa kuja uwanjani..!"
Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyowekwa kambani na Raphael Daudi aliyefunga la kwanza na Emanuel Martin aliyefunga bao la pili.
Yanga itahitaji sare au kufungwa bao 1-0 kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya makundi.
Iwapo itapata bao la ugenini itailazimu Dicha kushinda kwa mabao manne ifuzu.

ADVERTISE HERE