Katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu, Kennedy Musonda amedhihirisha umuhimu wake katika kikosi cha Yanga
Yawezekana katika ligi ya ndani anapata ukosoaji mwingi kwa kuwa hajafanya makubwa tangu atue Yanga lakini tangu msimu uliopita katika michuano ya kombe la Shirikisho, Musonda alidhihirisha ni mchezaji wa mechi kubwa
Katika kampeni ya ligi ya mabingwa msimu huu, Musonda amepachika mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao
Ukizungumzia wachezaji waliong'ara katika mechi mbili za robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns, Musonda ni miongoni mwao
Hata bao alilofunga Aziz Ki ambalo hata hivyo lilikataliwa na waamuzi, ilikuwa kazi nzuri kutoka kwa Musonda ambaye alipokea pasi kutoka kwa Aziz na kukimbia na mpira mpaka ndani ya eneo la hatari kisha kumrejeshea Aziz aliyetumbukiza mpira kimiani
Ni bahati mbaya tu, CAF hawakuwa tayari kuona Yanga inasonga mbele katika michuano hiyo hasa ikizingatiwa Rais wa Shirikisho hilo Patrice Motsepe ndiye mmiliki wa Sundowns
Katika wachezaji ambao wanastahili kuongezwa mikataba mipya na Yanga basi Musonda ni miongoni mwao