Kuna kipindi Youthe Rostand alishambuliwa sana na mashabiki kuwa hana uwezo na hastahili kulinda milingoti miwili ya goli la Yanga.
Lakini amekuwa akiwanyamazisha wakosoaji wake mmoja baada ya mwingine kutokana na kiwango anacho-onyesha mechi hadi mechi.
Rostand anaonekana kuimarika zaidi kila mchezo. Kwa sasa nadhani ndiye mlinda lango bora katika ardhi ya Tanzania.
Wapo makipa wengi Tanzania wanaofanya vizuri lakini Rostand ndiye kipa bora kwa sasa. Umbo lake linampa faida ya kuwazidi wengine.
Tumeshuhudia kazi kubwa aliyoifanya kwenye mchezo dhidi ya Wolaitta Dicha, aliokoa magoli kadhaa ya wazi.
Sasa anaonekana kuwa mkali, hataki masihara awapo langoni. Amekuwa kiongozi wa safu ya ulinzi, anatekeleza ipasavyo jukumu la kuwapanga walinzi wake.
Uwepo wake kwenye kikosi cha Yanga wakati huu utazidi kumuimarisha kinda Ramadhani Kabwili ambaye bila shaka siku za usoni ndiye atakayerithi mikoba yake.

ADVERTISE HERE